FAQ   |   Webmail
  • All children have equal rights
  • All children should be encouraged to fulfill their potential
  • Everybody has a responsibility to support the care and protection of children.
  • The child's views should be taken into account where major decisions are to be made about his or her future
  • Organizations working with children have a duty to care for children
Recent News
Events Calendar
Photo Gallery

Album:           TDH-MWANZA

Description: KIWOHEDE ni shirika lisilo la kiserikali linalotekeleza miradi yake kwa mbele juhudi zake za kuzuia biashara haramu ya usafirishaji wa binadam, dhuluma, unyanyasaji na unyonyaji ikiwa ni pamoja na shughuli ambazo zinalenga kutetea haki za watoto, uokoaji, na uwezeshaji kiuchumi kwa watoto ikiwa ni pamoja na utoaji wa stadi za maisha, mafunzo msaada wa kisheria, ushauri nasaha, huduma za matibabu, na kuwaunganisha na familia zao. MAELEZO YA SHUGHULI Utoaji wa huduma za elimu kwa watoto walio katika hatari na wahanga wa usafirishwaji unalenga kusaidia watoto waliobainiwa na kuokolewa kutoka katika usafirishwaji haramu na watoto kutoka katika familia zenye historia ya usafirishaji wa watoto. Kiwohede imekuwa ikisaidia watoto hawa kwa kuwaunganisha katika shule za msingi, sekondari na mafunzo ya ufundi kulingana na umri na sifa nyingine. Vyuo vya mafunzo ya ufundi ambavyo viko katika mkataba na shirika la KIWOHEDE na ambavyo watoto wamekuwa wakipelekwa ni pamoja na chuo cha mafunzo ya ufundi Buhongwa, chuo cha mafunzo ya ufundi St. Joseph, chuo cha mafunzo ya ufundi Nyakato, SIDO na Dar-es-salaam Chuo cha teknolojia (DIT) Mwanza pamoja na chuocha maendeleo ya jamii Sengerema (FDC). VIGEZO VYA UTEUZI  Mtoto lazima awe ameokolewa/ muhanga wa usafirishwaji haramu.  lazima awe katika katika hatari ya kusafirishwa  lazima awe na uwezo wa kusoma na kuandika MALENGO MAALUM. • Kutoa mafunzo ya ufundi stadi, elimu msingi na sekondari kwa watoto waathirika wa usafirishwaji haramu kama juhudi za kuwawezesha kiuchumi na kuwaepusha na kusafirishwa tena • Kuzuia ushiriki wa watoto katika kazi za hatari kama vile ukahaba, ajira za utotoni ambazo zinajumuisha kazi za ndani, Uvuvi, madini kwa kuwa na maarifa na ujuzi ambao utarahisisha uwezo wa kujiajiri. • Kuwawezesha watoto kiuchumi • Kutoa stadi za kujiajiri kwa watoto

Album Pictures

Design and Programming By : YouFly Co Limited Copyright © 2020 . KIWOHEDE. All Right Reserve.